Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 9:17-23 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Fikirini na kuwaita wanawake waomboleze;naam, waiteni wanawake hodari wa kuomboleza.

18. Waambieni: ‘Njoni hima mkaomboleze juu yetu,macho yetu yapate kuchuruzika machozi,na kope zetu zibubujike machozi kama maji.’”

19. Kilio kinasikika Siyoni:“Tumeangamia kabisa!Tumeaibishwa kabisa!Lazima tuiache nchi yetu,maana nyumba zetu zimebomolewa!

20. Enyi wanawake, sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu!Tegeni masikio msikie jambo analosema.Wafundisheni binti zenu kuomboleza,na jirani zenu wimbo wa maziko:

21. ‘Kifo kimepenya madirisha yetu,kimeingia ndani ya majumba yetu;kimewakatilia mbali watoto wetu barabarani,vijana wetu katika viwanja vya mji.

22. Maiti za watu zimetapakaa kila mahalikama marundo ya mavi mashambani,kama masuke yaliyoachwa na mvunaji,wala hakuna atakayeyakusanya.’Ndivyo alivyoniambia Mwenyezi-Mungu niseme.”

23. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Mwenye hekima asijivunie nguvu zake,wala tajiri asijivunie utajiri wake.

Kusoma sura kamili Yeremia 9