Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 9:10-16 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Nitaililia na kuiomboleza milima;nitayaombolezea malisho nyikani,kwa sababu yamekauka kabisa,hakuna mtu apitaye mahali hapo.Hakusikiki tena sauti za ng'ombe;ndege na wanyama wamekimbia na kutoweka.

11. Mwenyezi-Mungu asema:“Nitaifanya Yerusalemu magofu matupu,naam, nitaifanya kuwa pango la mbweha;na miji ya Yuda nitaifanya kuwa jangwa,mahali pasipokaliwa na mtu yeyote.”

12. Nami nikauliza, “Je kuna mtu mwenye hekima kiasi cha kuweza kueleza mambo haya? Mwenyezi-Mungu aliongea na nani hata huyo aweze kutangaza kitu hicho? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa tupu kama jangwa hata hakuna mtu apitaye humo?”

13. Mwenyezi-Mungu akajibu: “Kwa kuwa wamekataa kushika sheria yangu niliyowapa, wamekataa kutii sauti yangu na kufuata matakwa yake.

14. Badala yake wamefuata kwa ukaidi fikira za mioyo yao, wakaenda kuyaabudu Mabaali kama walivyofundishwa na wazee wao.

15. Basi, mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, nasema hivi: Tazama nitawalisha watu hawa uchungu na kuwapa maji yenye sumu wanywe.

16. Nitawatawanya kati ya mataifa ambayo wao wenyewe wala wazee wao hawakupata kuyajua; nitawafanya waandamwe na vita mpaka hapo nitakapowaangamiza wote.”

Kusoma sura kamili Yeremia 9