Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 9:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Laiti kichwa changu kingekuwa kisima cha maji,na macho yangekuwa chemchemi ya machoziili nipate kulia mchana na usiku,kwa ajili ya watu wangu waliouawa!

2. Laiti ningekuwa na mahali pa kukaa jangwani,ambamo ningewaacha watu wangu na kwenda zangu.”Mwenyezi-Mungu asema:“Wote ni watu wazinzi,ni genge la watu wahaini.

3. Hupinda maneno yao kama pinde;wameimarika kwa uongo na si kwa haki.Huendelea kutoka uovu hata uovu,wala hawanitambui mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

4. Kila mmoja ajihadhari na jirani yake!Hata ndugu yeyote haaminiki,kila ndugu ni mdanganyifu,na kila jirani ni msengenyaji.

5. Kila mmoja humdanganya jirani yake,hakuna hata mmoja asemaye ukweli.Wamezifundisha ndimi zao kusema uongo;hutenda uovu kiasi cha kushindwa kabisa kutubu.

6. Wanarundika dhuluma juu ya dhuluma,na udanganyifu juu ya udanganyifu.Wanakataa kunitambua mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

7. Kwa hiyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema:Tazama, nitawayeyusha na kuwajaribu!Au, nifanye nini zaidi na watu wangu waovu?

8. Ndimi zao ni kama mishale yenye sumu,daima haziishi kudanganya;kila mmoja huongea vema na jirani yake,lakini moyoni mwake hupanga kumshambulia.

9. Je, nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya?Je, nisilipe kisasi kwa taifa kama hili?Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

10. Nitaililia na kuiomboleza milima;nitayaombolezea malisho nyikani,kwa sababu yamekauka kabisa,hakuna mtu apitaye mahali hapo.Hakusikiki tena sauti za ng'ombe;ndege na wanyama wamekimbia na kutoweka.

11. Mwenyezi-Mungu asema:“Nitaifanya Yerusalemu magofu matupu,naam, nitaifanya kuwa pango la mbweha;na miji ya Yuda nitaifanya kuwa jangwa,mahali pasipokaliwa na mtu yeyote.”

12. Nami nikauliza, “Je kuna mtu mwenye hekima kiasi cha kuweza kueleza mambo haya? Mwenyezi-Mungu aliongea na nani hata huyo aweze kutangaza kitu hicho? Kwa nini nchi imeharibiwa na kufanywa tupu kama jangwa hata hakuna mtu apitaye humo?”

Kusoma sura kamili Yeremia 9