Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 51:2-19 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Nitawapeleka wapepetaji Babuloni,nao watampepeta;watamaliza kila kitu katika nchi yakewatakapofika kuishambulia toka kila upandewakati wa maangamizi yake.”

3. Usiwape nafasi wapiga mshale wa Babuloni;usiwaache wavute upinde,wala kuvaa mavazi yao ya vita.Usiwahurumie vijana wake;liangamize kabisa jeshi lake.

4. Wataanguka na kuuawa katika nchi ya Wakaldayo,watajeruhiwa katika barabara zake.

5. Lakini Israeli na Yuda hawakuachwa na Mungu wao Mwenyezi-Mungu wa majeshi,ingawa nchi yao imejaa hatia mbele yake yeye Mtakatifu wa Israeli.

6. Kimbieni kutoka Babuloni,kila mtu na ayaokoe maisha yake!Msiangamizwe katika adhabu yake,maana huu ndio wakati wa Mungu wa kulipa kisasi,anaiadhibu Babuloni kama inavyostahili.

7. Babuloni ilikuwa kikombe cha dhahabumkononi mwa Mwenyezi-Mungu,ambacho kiliilewesha dunia nzima.Mataifa yalikunywa divai yake,hata yakapatwa wazimu.

8. Ghafla Babuloni imeanguka na kuvunjikavunjika;ombolezeni kwa ajili yake!Leteni dawa kutuliza maumivu yake;labda utaweza kuponywa.

9. Tulijaribu kuuponya Babuloni,lakini hauwezi kuponywa.Uacheni, twendeni zetu,kila mmoja katika nchi yake,maana hukumu yake ni kuu mnoimeinuka mpaka mawinguni.

10. Mwenyezi-Mungu amethibitisha kuwa hatuna hatia.Twendeni Siyoni tukatangazematendo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.

11. Mwenyezi-Mungu amezichochea roho za wafalme wa Media, kwa maana amenuia kuiangamiza Babuloni. Naam, hicho ndicho kisasi cha Mwenyezi-Mungu; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.Noeni mishale yenu!Chukueni ngao!

12. Twekeni bendera ya vitakushambulia kuta za Babuloni.Imarisheni ulinzi;wekeni walinzi;tayarisheni mashambulizi.Mwenyezi-Mungu amepanga na kutekelezamambo aliyosema juu ya wakazi wa Babuloni.

13. Nchi hiyo imejaa mito na hazina tele,lakini mwisho wake umefika,uzi wa uhai wake umekatwa.

14. Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa kwa nafsi yake:“Hakika nitakujaza majeshi mengi kama nzige,nayo yatapiga vigelegele vya ushindi juu yako”

15. Mwenyezi-Mungu ndiye aliyeumba dunia kwa nguvu yake,aliyeuimarisha ulimwengu kwa hekima yake,na kwa maarifa yake akazitandaza mbingu.

16. Anapotoa sauti yake maji hutitima mbinguni,hufanya ukungu upande kutoka mipaka ya dunia.Hufanya umeme umulike wakati wa mvuahuvumisha upepo kutoka ghala zake.

17. Kila mtu ni mpumbavu bila maarifa,kila mhunzi anaaibishwa na vinyago vyake;maana sanamu zake ni udanganyifu mtupu,wala hazina pumzi ndani yake.

18. Hazina thamani, ni udanganyifu mtupu;wakati watakapoadhibiwa,nazo zitaangamia.

19. Mungu aliye hazina ya Yakobo si kama hizo,maana yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote,na Israeli ni kabila lililo mali yake;Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, ndilo jina lake.

Kusoma sura kamili Yeremia 51