Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 51:10-27 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Mwenyezi-Mungu amethibitisha kuwa hatuna hatia.Twendeni Siyoni tukatangazematendo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu.

11. Mwenyezi-Mungu amezichochea roho za wafalme wa Media, kwa maana amenuia kuiangamiza Babuloni. Naam, hicho ndicho kisasi cha Mwenyezi-Mungu; analipiza kisasi kwa ajili ya hekalu lake.Noeni mishale yenu!Chukueni ngao!

12. Twekeni bendera ya vitakushambulia kuta za Babuloni.Imarisheni ulinzi;wekeni walinzi;tayarisheni mashambulizi.Mwenyezi-Mungu amepanga na kutekelezamambo aliyosema juu ya wakazi wa Babuloni.

13. Nchi hiyo imejaa mito na hazina tele,lakini mwisho wake umefika,uzi wa uhai wake umekatwa.

14. Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa kwa nafsi yake:“Hakika nitakujaza majeshi mengi kama nzige,nayo yatapiga vigelegele vya ushindi juu yako”

15. Mwenyezi-Mungu ndiye aliyeumba dunia kwa nguvu yake,aliyeuimarisha ulimwengu kwa hekima yake,na kwa maarifa yake akazitandaza mbingu.

16. Anapotoa sauti yake maji hutitima mbinguni,hufanya ukungu upande kutoka mipaka ya dunia.Hufanya umeme umulike wakati wa mvuahuvumisha upepo kutoka ghala zake.

17. Kila mtu ni mpumbavu bila maarifa,kila mhunzi anaaibishwa na vinyago vyake;maana sanamu zake ni udanganyifu mtupu,wala hazina pumzi ndani yake.

18. Hazina thamani, ni udanganyifu mtupu;wakati watakapoadhibiwa,nazo zitaangamia.

19. Mungu aliye hazina ya Yakobo si kama hizo,maana yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote,na Israeli ni kabila lililo mali yake;Mwenyezi-Mungu wa Majeshi, ndilo jina lake.

20. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Wewe Babuloni ni rungu na silaha yangu ya vita;nakutumia kuyavunjavunja mataifa,nakutumia kuangamiza falme.

21. Nakutumia kuponda farasi na wapandafarasi,magari ya kukokotwa na waendeshaji wake.

22. Ninakutumia kuwaponda wanaume na wanawake,wazee na vijana,wavulana na wasichana.

23. Ninakutumia kuponda wachungaji na makundi yao,wakulima na wanyama wao wa kulimia,wakuu wa mikoa na madiwani.

24. “Nitaiadhibu Babuloni na wakazi wote wa Kaldayo mkiona kwa macho yenu wenyewe, kwa sababu ya uovu wote walioufanya katika Siyoni. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

25. Mimi ninapingana nawe ewe mlima mharibifu,mlima unaoharibu dunia nzima!Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.Nitanyosha mkono wangu dhidi yako,nitakuangusha kutoka miambani juuna kukufanya kuwa mlima uliochomwa moto;

26. hata hamna jiwe lako litakalochukuliwa kujengea,hakuna jiwe litakalochukuliwa kuwekea msingi!Utakuwa kama jangwa milele.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

27. Tweka bendera ya vita duniani,piga tarumbeta kati ya mataifa;yatayarishe mataifa kupigana naye;ziite falme kuishambulia;falme za Ararati, Mini na Ashkenazi.Weka majemadari dhidi yake;walete farasi kama makundi ya nzige.

Kusoma sura kamili Yeremia 51