Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 50:9-16 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Maana, mimi nitachochea mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini washambulie Babuloni. Watajiandaa kuishambulia Babuloni na kuiteka. Mishale yao ni kama shujaa hodari asiyerudi mikono mitupu.

10. Nchi ya Wakaldayo itaporwa, na hao watakaoipora wataridhika. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

11. “Enyi waporaji wa mali yangu!Japo mnafurahi na kushangilia,mnarukaruka kama mtamba wa ng'ombe anayepura nafaka,na kulia kama farasi dume,

12. nchi yenu ya kuzaliwa itaaibishwa;hiyo nchi mama yenu itafedheheshwa.Lo! Babuloni itakuwa ya mwisho kati ya mataifa,itakuwa nyika kame na jangwa.

13. Kwa sababu ya ghadhabu yangu Mwenyezi-Mungu,Babuloni haitakaliwa kabisa na watu,bali itakuwa jangwa kabisa;kila atakayepita karibu nayo atashangaaataizomea kwa sababu ya majeraha yake.

14. “Enyi nyote wapiga mishale stadi,shikeni nafasi zenu kuuzingira mji wa Babuloni;upigeni, msibakize mshale hata mmoja,maana umenikosea mimi Mwenyezi-Mungu.

15. Upigieni kelele za vita pande zote,sasa Babuloni umejitoa ukamatwe.Ngome zake zimeanguka,kuta zake zimebomolewa.Ninalipiza kisasi juu ya BabuloniBasi jilipizeni kisasi,utendeeni kama ulivyowatenda wengine.

16. Zuieni watu wasipande mbegu Babuloni,wala wasivune wakati wa mavuno.Kutokana na upanga wa udhalimu,kila mmoja atawarudia watu wakekila mmoja atakimbilia nchini mwake.

Kusoma sura kamili Yeremia 50