Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 49:1-13 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kuhusu Waamoni.Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Je, Israeli hana watoto?Je, hana warithi?Mbona basi mungu Milkomu amemiliki Gadina watu wake kufanya makao yao mijini mwake?

2. Basi, wakati unakuja kweli, siku zaja,nasema mimi Mwenyezi-Mungu,ambapo nitavumisha sauti ya vitadhidi ya Raba mji wa Waamoni.Raba utakuwa rundo la uharibifu,vijiji vyake vitateketezwa moto;ndipo Israeli atakapowamiliki wale waliomiliki.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

3. “Ombolezeni, enyi watu wa Heshboni,maana mji wa Ai umeharibiwa!Lieni enyi binti za Raba!Jifungeni mavazi ya gunia viunoniombolezeni na kukimbia huko na huko uani!Maana mungu Milkomu atapelekwa uhamishoni,pamoja na makuhani wake na watumishi wake.

4. Mbona mnajivunia mabonde yenu, enyi msioamini,watu mliotegemea mali zenu, mkisema:‘Nani atathubutu kupigana nasi?’

5. Basi, mimi nitawaleteeni vitishokutoka kwa jirani zenu wote,nanyi mtafukuzwa nje kila mtu kivyake,bila mtu wa kuwakusanya wakimbizi.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.

6. Lakini baadaye nitawarudishia Waamoni fanaka yao.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

7. Kuhusu Edomu.Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi:“Je, hakuna tena hekima mjini Temani?Je, wenye busara wao hawana shauri tena?Hekima imetoweka kabisa?

8. Kimbieni enyi wakazi wa Dedani;geukeni mkaishi mafichoni!Maana nitawaleteeni maangamizienyi wazawa wa Esau;wakati wa kuwaadhibu umefika.

9. Wachuma zabibu watakapokuja kwenuhawatabakiza hata zabibu moja.Usiku ule wezi watakapofika,wataharibu kila kitu mpaka watosheke.

10. Lakini nimemnyanganya Esau kila kitu,naam, nimeyafunua maficho yake,wala hawezi kujificha tena.Watoto, ndugu na jirani zake wameangamizwa;hakuna hata mmoja aliyebaki.

11. Niachieni watoto wenu yatima nami nitawatunza;waacheni wajane wenu wanitegemee.”

12. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ikiwa wale ambao hawakustahili kunywa kikombe cha adhabu ni lazima wanywe, je, wewe utaachwa bila kuadhibiwa? La! Hutakosa kuadhibiwa; ni lazima unywe hicho kikombe!

13. Maana nimeapa kwa nafsi yangu kwamba mji wa Bosra utakuwa kioja na kichekesho, utakuwa uharibifu na laana; vijiji vyote vitakuwa magofu daima. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

Kusoma sura kamili Yeremia 49