Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 46:15-24 Biblia Habari Njema (BHN)

15. Kwa nini shujaa wako amekimbia?Mbona fahali wako hakuweza kustahimili?Kwa sababu mimi Mwenyezi-Mungu nilimwangusha chini!

16. Wengi walijikwaa, wakaanguka,kisha wakaambiana wao kwa wao:‘Simameni, tuwaendee watu wetu,turudi katika nchi yetu,tuukimbie upanga wa adui.’

17. “Naye Farao, mfalme wa Misri, mpangeni jina hili:‘Kishindo kitupu!’

18. Mimi naapa kwa uhai wangunasema mimi mfalme niitwaye Mwenyezi-Mungu wa majeshi,kweli adui anakuja kuwashambulieni:Ni hakika kama Tabori ulivyo mlimakama mlima Karmeli uonekanavyo kutoka baharini.

19. Enyi wakazi wa Misrijitayarisheni na mizigo kwenda uhamishoni!Maana mji wa Memfisi utaharibiwa kabisa,utakuwa magofu yasiyokaliwa na watu.

20. Misri ni kama mtamba mzuri wa ng'ombe,lakini kipanga kutoka kaskazini amemvamia.

21. Hata askari wake wa kukodiwa ni kama ndama wanono;nao pia wamegeuka, wakakimbia pamoja,wala hawakuweza kustahimili,kwa maana siku yao ya kuangamizwa imefika,wakati wao wa kuadhibiwa umewadia.

22. Misri anatoa sauti kama nyoka anayekimbia;maana maadui zake wanamjia kwa nguvu,wanamjia kwa mashoka kama wakata-miti.

23. Wataukata kabisa msitu wake, ingawa haupenyeki,nasema mimi Mwenyezi-Mungu,maana wao ni wengi kuliko nzige wasiohesabika.

24. Watu wa Misri wataaibishwa,watatiwa mikononi mwa watu kutoka kaskazini.”

Kusoma sura kamili Yeremia 46