Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 40:14-16 Biblia Habari Njema (BHN)

14. “Je, una habari kwamba Baali mfalme wa Waamoni, amemtuma Ishmaeli mwana wa Nethania, akuue?” Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu, hakuamini maneno yao.

15. Kisha, Yohanani mwana wa Karea, akazungumza na Gedalia kwa faragha huko Mizpa, akamwambia, “Acha niende nikamuue Ishmaeli mwana wa Nethania, na hakuna mtu yeyote atakayejua. Kwa nini yeye akuue na watu wa Yuda wote waliokusanyika hapa watawanyike na Wayahudi waliobaki waangamie?”

16. Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu, akamwambia Yohanani mwana wa Karea, “Usifanye jambo hilo! Mambo unayosema juu ya Ishmaeli si ya kweli!”

Kusoma sura kamili Yeremia 40