Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 3:5-13 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Je, utanikasirikia daima?Utachukizwa nami milele?’Israeli, hivyo ndivyo unavyosema;na kumbe umetenda uovu wote ulioweza.”

6. Wakati wa utawala wa mfalme Yosia, Mwenyezi-Mungu aliniambia hivi: “Je, umeona jinsi Israeli asiye mwaminifu alivyofanya? Aliniacha, akapanda juu ya kila kilima kirefu na kwenda chini ya kila mti wenye majani mabichi, akafanya ukahaba wake humo!

7. Mimi nilidhani kuwa baada ya kufanya yote hayo, atanirudia. Lakini wapi; hakunirudia. Yuda, dada yake mdanganyifu, alishuhudia yote hayo.

8. Zaidi ya hayo, Yuda alishuhudia kuwa nilimpa Israeli talaka kwa sababu ya ukahaba wake na kwa kukosa uaminifu kwangu. Lakini hata hivyo, Yuda, dada yake mdanganyifu, hakuogopa; naye pia alikwenda na kufanya ukahaba!

9. Na, kwa kuwa yeye aliona kuwa ukahaba ni jambo dogo sana kwake, aliitia nchi unajisi, na kufanya ukahaba kwa kuabudu mawe na miti.

10. Pamoja na hayo yote, Yuda, dada mdanganyifu wa Israeli, hakunirudia kwa moyo wote, bali kwa unafiki tu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”

11. Mwenyezi-Mungu akaniambia, “Mwasi Israeli amedhihirisha kuwa yeye ni afadhali kuliko Yuda mdanganyifu.

12. Basi, nenda ukamtangazie Israeli maneno yafuatayo:Rudi, ewe Israeli, usiye mwaminifu.Nami sitakutazama kwa hasirakwa kuwa mimi ni mwenye huruma.Naam, sitakukasirikia milele.

13. Wewe, kiri tu kosa lako:Kwamba umeniasi mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako;kwamba chini ya kila mti wenye majani,umewapa miungu wengine mapenzi yakowala hukuitii sauti yangu.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Kusoma sura kamili Yeremia 3