Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 20:7-15 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umenidanganya,nami kweli nikadanganyika;wewe una nguvu kuliko mimi,nawe umeshinda.Kutwa nzima nimekuwa mtu wa kuchekwa,kila mtu ananidhihaki.

8. Kila ninaposema kitu, nalalamika,napaza sauti, “Ukatili na uharibifu!”Maana kwangu kutangaza neno la Mwenyezi-Mungukwanifanya nishutumiwe na kudhihakiwa kutwa nzima.

9. Lakini nikisema, “Sitamtaja Mwenyezi-Mungu,wala sitasema tena kwa jina lake,”moyoni mwangu huwa na kitu kama moto uwakao,uliofungiwa ndani ya mifupa yangu.Najaribu sana kuuzuia humo,lakini ninashindwa.

10. Nasikia wengi wakinongona juu yangu.Wananipanga jina: “Kitisho kila upande!”Wengine wanasema:“Nendeni mkamshtaki! Na tumshtaki!”Hata rafiki zangu wote wapenzi wanangojea tu nianguke!Wanasema “Labda atadanganyika, nasi tutalipiza kisasi.”

11. Lakini wewe Mwenyezi-Mungu u pamoja namikwangu wewe ni kama shujaa wa kutisha;kwa hiyo watesi wangu watajikwaa,na hawataweza kunishinda.Wataaibika kupindukia,maana hawatafaulu.Fedheha yao itakuwa ya daima;kamwe haitasahaulika.

12. Ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi,wewe humthibiti mtu mwadilifu,huona yaliyo moyoni na akilini mwa watu,unijalie kuona ukiwalipiza kisasi,maana kwako nimekiweka kisa changu.

13. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu;msifuni Mwenyezi-Mungu,kwani ameyaokoa maisha ya mhitaji,kutoka mikononi mwa watu waovu.

14. Na ilaaniwe siku niliyozaliwa!Siku hiyo mama aliponizaa,isitakiwe baraka!

15. Na alaaniwe aliyempelekea baba ujumbe:“Umepata mtoto wa kiume”,akamfanya ajae furaha.

Kusoma sura kamili Yeremia 20