Agano la Kale

Agano Jipya

Yeremia 2:12-19 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Shangaeni enyi mbingu, juu ya jambo hili,mkastaajabu na kufadhaika kabisa.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

13. Maana, watu wangu wametenda maovu mawili;wameniacha mimi niliye chemchemi ya maji ya uhai,wakajichimbia visima vyao wenyewe,visima vyenye nyufa, visivyoweza kuhifadhi maji.

14. “Je, Israeli ni mtumwa,ama amezaliwa utumwani?Mbona basi amekuwa kama mawindo?

15. Simba wanamngurumia,wananguruma kwa sauti kubwa.Nchi yake wameifanya jangwa,miji yake imekuwa magofu, haina watu.

16. Isitoshe, watu wa Memfisi na Tahpanesi,wameuvunja utosi wake.

17. Israeli, je, hayo yote si umejiletea mwenyewe,kwa kuniacha mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,niliyekuwa ninakuongoza njiani?

18. Na sasa itakufaa nini kwenda Misri,kunywa maji ya mto Nili?Au itakufaa nini kwenda Ashuru,kunywa maji ya mto Eufrate?

19. Uovu wako utakuadhibu;na uasi wako utakuhukumu.Ujue na kutambua kuwa ni vibaya mnokuniacha mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako,na kuondoa uchaji wangu ndani yako.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.

Kusoma sura kamili Yeremia 2