Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 8:8-14 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Tunaye dada mdogo,ambaye bado hajaota matiti.Je, tumfanyie nini dada yetusiku atakapoposwa?

9. Kama angalikuwa ukuta,tungalimjengea mnara wa fedha;na kama angalikuwa mlango,tungalimhifadhi kwa mbao za mierezi.

10. Mimi nalikuwa ukuta,na matiti yangu kama minara yake.Machoni pake nalikuwakama mwenye kuleta amani.

11. Solomoni alikuwa ana shamba la mizabibu,mahali paitwapo Baal-hamoni.Alilikodisha kwa walinzi;kila mmoja wao alilipa vipande elfu vya fedha.

12. Shamba langu la mizabibu ni shamba langu mwenyewe,naam, ni shamba langu binafsi!Basi, Solomoni, wewe ukae na elfu zako za fedha,na kila mlinzi wa matunda akae na mia mbili zake.

13. Ewe uliye shambani,rafiki zangu wanasikiliza sauti yako;hebu nami niisikie tafadhali!

14. Njoo haraka ewe mpenzi wangu,kama paa au mwanapaa dume juu ya milima ya manukato.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 8