Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 8:12-14 Biblia Habari Njema (BHN)

12. Shamba langu la mizabibu ni shamba langu mwenyewe,naam, ni shamba langu binafsi!Basi, Solomoni, wewe ukae na elfu zako za fedha,na kila mlinzi wa matunda akae na mia mbili zake.

13. Ewe uliye shambani,rafiki zangu wanasikiliza sauti yako;hebu nami niisikie tafadhali!

14. Njoo haraka ewe mpenzi wangu,kama paa au mwanapaa dume juu ya milima ya manukato.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 8