Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 8:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Laiti ungekuwa kaka yangu,ambaye amenyonyeshwa na mama yangu!Hivyo, hata kama ningekutana nawe nje,ningekubusu na hakuna ambaye angenidharau.

2. Ningekuongoza na kukufikisha nyumbani kwa mama mzazi,mahali ambapo ungenifundisha upendo.Ningekupa divai nzuri iliyokolezwa,ningekupa divai yangu ya makomamanga yangu.

3. Mkono wako wa kushoto u chini ya kichwa changu,na mkono wako wa kulia wanikumbatia.

4. Nawasihini, enyi wanawake wa Yerusalemu,msiyachochee wala kuyaamsha mapenzi,hadi hapo wakati wake utakapofika.

5. Ni nani huyu ajaye kutoka mbugani,huku anamwegemea mpenzi wake?Chini ya mtofaa, mimi nilikuamsha,pale ambapo mama yako aliona uchungu,naam, pale ambapo mama yako alikuzaa.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 8