Agano la Kale

Agano Jipya

Wimbo Ulio Bora 5:10-16 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Mpenzi wangu ni mzuri na mwenye nguvu,mashuhuri miongoni mwa wanaume elfu kumi.

11. Kichwa chake kizuri kama dhahabu safi,nywele zake ni za ukoka,nyeusi ti kama kunguru.

12. Macho yake ni kama ya hua kandokando ya kijito,ni kama njiwa waliooga maziwa kando ya kijito.

13. Mashavu yake ni kama matuta ya rihanikama bustani iliyojaa manukato na manemane.Midomo yake ni kama yungiyungi,imelowa manemane kwa wingi.

14. Mikono yake imewekwa bangili za dhahabu,amevalia johari za Tarshishi.Kiwiliwili chake ni kama pembe za ndovuzilizopambwa kwa vito vya johari ya rangi ya samawati.

15. Miguu yake ni kama nguzo za alabastazilizosimikwa katika misingi ya dhahabu.Umbo lake ni kama Lebanoni,ni bora kama miti ya mierezi.

16. Kinywa chake kimejaa maneno matamu,kwa ujumla anapendeza.Basi, hivyo ndivyo alivyo mpenzi wangu,naam, ndivyo alivyo rafiki yangu,enyi wanawake wa Yerusalemu.

Kusoma sura kamili Wimbo Ulio Bora 5