Agano la Kale

Agano Jipya

Walawi 3:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Kama mtu anatoa sadaka ya amani, na sadaka yake ni ng'ombe dume au jike basi, mnyama huyo asiwe na dosari mbele yangu.

2. Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mnyama huyo na kumchinja mlangoni mwa hema la mkutano. Hao makuhani wazawa wa Aroni watainyunyizia madhabahu damu yake pande zake zote.

3. Mafuta yote yanayofunika na yaliyo juu ya matumbo ya mnyama wa sadaka hiyo ya amani atayateketeza kama sadaka anayotolewa Mwenyezi-Mungu kwa moto.

4. Atatoa pia zile figo mbili na mafuta yake pamoja na ile sehemu bora ya ini.

5. Wazawa wa Aroni wataiteketeza madhabahuni pamoja na sadaka ya kuteketezwa iliyoko juu ya kuni; hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Walawi 3