Agano la Kale

Agano Jipya

Walawi 17:8-15 Biblia Habari Njema (BHN)

8. “Waambie kwamba mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli au mgeni anayeishi kati yao, anayetoa sadaka ya kuteketezwa au tambiko,

9. lakini haileti mbele ya mlango wa hema la mkutano ili kumtolea Mwenyezi-Mungu, mtu huyo atatengwa na watu wake.

10. “Kama mtu yeyote wa jumuiya ya Israeli au mgeni anayeishi kati yao anakula damu yoyote, mimi nitamwandama mtu huyo aliyekula damu na kumtenga mbali na watu wake.

11. Itakuwa hivyo kwa sababu uhai wa kiumbe umo katika damu. Nimewaagiza kuitolea damu madhabahuni ili kufanya ibada ya upatanisho kwa ajili ya roho zenu; kwa sababu damu hufanya upatanisho maana uhai umo katika damu.

12. Ndiyo maana nimewaagiza Waisraeli hivi: Mtu yeyote miongoni mwenu wala mgeni anayeishi kati yenu kamwe asile damu.

13. “Mtu yeyote miongoni mwa Waisraeli au mgeni anayekaa miongoni mwao akienda kuwinda mnyama au ndege, ni lazima aimwage damu chini na kuifunika kwa udongo.

14. Maana, uhai wa kila kiumbe umo katika damu. Ndiyo maana nimewaagiza Waisraeli, kamwe wasile damu ya kiumbe chochote kwani uhai wa kiumbe chochote ni damu yake. Yeyote atakayekula damu atatengwa.

15. “Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni, anayekula chochote kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, lazima ayafue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. Baada ya hapo atakuwa safi.

Kusoma sura kamili Walawi 17