Agano la Kale

Agano Jipya

Waamuzi 5:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Siku hiyo, Debora na Baraki, mwana wa Abinoamu, wakaimba wimbo huu:

2. “Viongozi walijitokeza kuongoza Israeli,watu walijitolea kwa hiari yao.Mshukuruni Mwenyezi-Mungu!

3. “Sikilizeni, enyi wafalme!Tegeni sikio, enyi wakuu!Nitamwimbia Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.

4. “Ee Mwenyezi-Mungu, ulipotoka huko Seiri,ulipoteremka mlimani Edomu,nchi ilitetemeka,mbingu zilidondosha maji,naam, mawingu yakaiangusha mvua.

5. Milima ilitikisika mbele yako Mwenyezi-Mungu,naam, mlima Sinai mbele yako Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli.

6. “Katika siku za Shamgari, mwana wa Anathi,katika wakati wa Yaeli,misafara ilikoma kupita nchini,wasafiri walipitia vichochoroni.

7. Wakulima walikoma kuwako,walikoma kuwako katika Israeli,mpaka nilipotokea mimi Debora,mimi niliye kama mama wa Israeli.

8. Walijichagulia miungu mipya,kukawa na vita katika nchi.Lakini hakukupatikana mwenye upanga au ngaokati ya watu 40,000 wa Israeli.

Kusoma sura kamili Waamuzi 5