Sura

  1. 1
  2. 2
  3. 3
  4. 4
  5. 5
  6. 6
  7. 7
  8. 8
  9. 9
  10. 10
  11. 11
  12. 12
  13. 13
  14. 14
  15. 15
  16. 16
  17. 17
  18. 18
  19. 19
  20. 20
  21. 21

Agano la Kale

Agano Jipya

Waamuzi 17 Biblia Habari Njema (BHN)

Sanamu za Mika

1. Kulikuwa na mtu mmoja huko katika milima ya Efraimu, jina lake Mika.

2. Siku moja alimwambia mama yake, “Vile vipande 1,100 vya fedha ulivyoibiwa, nawe ukamlaani aliyekuibia nikisikia, mimi ninavyo. Mimi ndiye niliyevichukua.” Mama yake akasema, “Mwanangu, ubarikiwe na Mwenyezi-Mungu.”

3. Mika akamrudishia mama yake hivyo vipande 1,100 vya fedha. Mama yake akasema, “Ili laana niliyotoa isikupate, fedha hii naiweka wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, ili kutengenezea sanamu ya kuchonga na ya kusubu. Sasa ninakurudishia vipande hivyo vya fedha.”

4. Mika alipomrudishia mama yake hiyo fedha, mama yake akachukua vipande 200 vya fedha, akampa mfua fedha, naye akafua sanamu ya kuchonga na ya kusubu. Sanamu hiyo ikawekwa ndani ya nyumba ya Mika.

5. Mtu huyo, Mika, alikuwa na mahali pake pa ibada. Alitengeneza kizibao cha kuhani na kinyago, kisha akamfanya mmoja wa watoto wake kuwa kuhani wake.

6. Siku hizo hapakuwepo na mfalme katika Israeli. Kila mtu alifanya chochote alichoona ni chema.

7. Wakati huo kulikuwa na kijana mmoja Mlawi mjini Bethlehemu nchini Yuda.

8. Kijana huyo akaondoka Bethlehemu nchini Yuda, akaenda kutafuta mahali pengine pa kuishi. Katika safari yake akafika nyumbani kwa Mika katika nchi ya milima ya Efraimu.

9. Mika akamwuliza, “Umetoka wapi?” Naye akamjibu, “Mimi ni Mlawi, kutoka mjini Bethlehemu nchini Yuda. Nitakaa popote nitakapopata nafasi ya kukaa kama mgeni.”

10. Mika akamwambia, “Kaa pamoja nami, uwe kwangu kama baba na kuhani wangu. Nitakulipa vipande kumi vya fedha kila mwaka na mavazi pamoja na mahitaji yako.”

11. Huyo Mlawi akaingia akakubali, akakaa huko na kuwa kama mmoja wa wana wa Mika.

12. Naye Mika akamfanya kijana huyo Mlawi kuwa kuhani wake huko nyumbani kwake.

13. Kisha akasema, “Sasa najua kwamba Mwenyezi-Mungu atanifanikisha kwani nina kijana huyu Mlawi kama kuhani wangu.”