Agano la Kale

Agano Jipya

Sefania 3:2-12 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Hausikilizi onyo lolote,wala haukubali kukosolewa.Haukumtegemea Mwenyezi-Mungu kamwe,wala kumkaribia Mungu wake.

3. Viongozi wake ni simba wangurumao,mahakimu wake ni mbwamwitu wenye njaa jioniwasioacha chochote mpaka asubuhi.

4. Manabii wake ni watu wasiojali na wadanganyifu.Makuhani wake wamevitia unajisi vitu vitakatifuna kuihalifu sheria kwa nguvu.

5. Lakini Mwenyezi-Mungu aliye mjini humo ni mwadilifu,yeye hatendi jambo lolote baya.Kila siku asubuhi hudhihirisha kauli yake,naam, kila kunapopambazuka huitekeleza.Lakini wahalifu hawana aibu hata kidogo.

6. Mwenyezi-Mungu asema:“Nimeyafutilia mbali mataifa;kuta zao za kujikinga ni magofu.Barabara zao nimeziharibu,na hamna apitaye humo.Miji yao imekuwa mitupu,bila watu, na bila wakazi.

7. Nilisema, ‘Hakika mji huu watanichana kukubali kukosolewa;hautaacha kukumbuka mara hizo zote nilizowaadhibu.’Lakini watu wake walizidisha tamaa zaoza kufanya matendo yao kuwa upotovu.

8. “Kwa hiyo ningojeni mimi Mwenyezi-Mungu,ngoja siku nitakapoinuka kutoa mashtaka.Nimeamua kuyakusanya mataifa na falme,kuyamwagia ghadhabu yangu,kadhalika na ukali wa hasira yangu.Dunia yote itateketezwakwa moto wa ghadhabu yangu.

9. “Wakati huo nitaibadili lugha ya watu,nitawawezesha kusema lugha adiliili waniite mimi Mwenyezi-Mungu,na kuniabudu kwa moyo mmoja.

10. Kutoka ng'ambo ya mito ya Kushiwatu wangu wanaoniomba ambao wametawanyika,wataniletea sadaka yangu.

11. “Siku hiyo, haitakulazimu kuona aibu,kutokana na matendo yako ya kuniasi,maana nitawaondoa miongoni mwakowale wanaojigamba na kujitukuzanawe hutakuwa na kiburi tena katika mlima wangu mtakatifu.

12. Nitakuachia watu wapole na wanyenyekevuambao watakimbilia usalama kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Sefania 3