1. Ole wake mji wa Yerusalemu,mji mchafu, najisi na mdhalimu.
2. Hausikilizi onyo lolote,wala haukubali kukosolewa.Haukumtegemea Mwenyezi-Mungu kamwe,wala kumkaribia Mungu wake.
3. Viongozi wake ni simba wangurumao,mahakimu wake ni mbwamwitu wenye njaa jioniwasioacha chochote mpaka asubuhi.