Agano la Kale

Agano Jipya

Sefania 1:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno la Mwenyezi-Mungu lililomjia Sefania mwana wa Kushi, mwana wa Gedalia, mwana wa Amenia, mwana wa Hezekia, wakati wa utawala wa mfalme Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda:

2. Mwenyezi-Mungu asema:“Nitavifagilia mbali viumbe vyote duniani:

3. Wanadamu, wanyama, ndege wa anganina samaki wa baharini;vyote nitaviangamiza.Waovu nitawaangamiza kabisa;wanadamu nitawafagilia mbali duniani.

4. Nitaunyosha mkono wangu dhidi ya nchi ya Yuda,kadhalika na wakazi wote wa mji wa Yerusalemu.Nitaangamiza mabaki yote ya Baali kutoka nchi hii,na hakuna atakayetambua jina lao.

5. Nitawaangamiza wote wanaosujudu juu ya paa,wakiabudu jeshi la mbinguni.Nitawaangamiza wale wanaoniabuduna kuapa kwa jina langu,hali wanaapa pia kwa jina la mungu Milkomu.

6. Nitawaangamiza wote walioniacha mimi Mwenyezi-Munguwote walioacha kunitafuta na kuniuliza shauri.”

Kusoma sura kamili Sefania 1