Agano la Kale

Agano Jipya

Ruthu 3:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Baada ya muda, Naomi mkwewe alimwambia Ruthu, “Ni wajibu wangu kukutafutia mume ili upate mema.

2. Sasa huyu Boazi, ambaye ulifanya kazi na wasichana wake, je, si ni wa ukoo wetu? Haya basi sikiliza, jioni hii atakuwa anapura shayiri.

3. Kwa hiyo, nawa, ujipake manukato na kuvalia vizuri, kisha uende mahali anapopuria; lakini angalia usitambulike kwake mpaka atakapomaliza kula na kunywa.

4. Pia, ujue mahali atakapolala, na akisha kusinzia, mwendee polepole uifunue miguu yake ulale papo hapo. Yeye atakueleza la kufanya.”

Kusoma sura kamili Ruthu 3