Agano la Kale

Agano Jipya

Ruthu 1:14-20 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Hapo walipaza sauti wakaanza kulia tena. Ndipo Orpa akamkumbatia mkwewe, akamuaga na kurudi nyumbani; lakini Ruthu, akaandamana naye.

15. Basi Naomi akamwambia, “Ruthu, tazama dada yako amerudi nyumbani kwake na kwa mungu wake; basi, nawe pia urudi, umfuate dada yako.”

16. Lakini Ruthu akamjibu,“Usinisihi nikuache wewe,wala usinizuie kufuatana nawe.Kokote utakakokwenda ndiko nami nitakakokwenda,na ukaapo nitakaa,watu wako watakuwa watu wangu,na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.

17. Pale utakapofia hapo nitakufa nami,na papo hapo nitazikwa;Mwenyezi-Mungu anipe adhabu kali kama nikitenganishwa naweisipokuwa tu kwa kifo.”

18. Naomi alipoona kuwa Ruthu ameamua kwenda pamoja naye, aliacha kumshawishi.

19. Ndipo wote wawili wakaendelea na safari hadi Bethlehemu. Walipofika huko, watu wote walishangaa, hata wanawake wakaulizana, “Je, huyu ni Naomi?”

20. Naomi akasema, “Msiniite tena Naomi niiteni Mara, kwa maana Mungu mwenye nguvu ameyafanya maisha yangu yawe machungu mno.

Kusoma sura kamili Ruthu 1