Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 11:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kisha, viongozi wa watu wakakaa mjini Yerusalemu; watu wengine wote, wakapiga kura kati ya kila jamaa kumi ili kuchagua jamaa moja itakayokaa mjini Yerusalemu, mji mtakatifu. Jamaa nyingine tisa zikakaa katika miji yao mingine.

2. Watu wakawasifu wale wote waliokubali kukaa mjini Yerusalemu.

3. Na katika miji mingine, watu wa Israeli, makuhani, Walawi, walinzi wa malango na wazawa wa watumishi wa Solomoni, walikaa katika maeneo yao wenyewe, katika miji yao.

4. Baadhi ya watu wa kabila la Yuda na wa kabila la Benyamini walikaa katika mji wa Yerusalemu. Wafuatao ndio watu wa ukoo wa Yuda waliokaa mjini Yerusalemu: Athaya, mwana wa Uzia, mwana wa Zekaria, mwana wa Amaria, mwana wa Shefatia, mwana wa Mahalaleli. Wote hao ni wazawa wa Peresi.

Kusoma sura kamili Nehemia 11