Agano la Kale

Agano Jipya

Nehemia 10:31-35 Biblia Habari Njema (BHN)

31. Ikiwa watu hao wanaleta bidhaa au nafaka kuuza siku ya Sabato, sisi hatutanunua siku hiyo wala siku nyingine yoyote iliyo takatifu. Mwaka wa saba hatutailima ardhi na madeni yote tutayafuta.

32. Tunajiwekea sheria kwamba kwa mwaka tutatoa theluthi moja ya shekeli kwa ajili ya gharama za huduma ya nyumba ya Mungu:

33. Mikate mitakatifu, sadaka za nafaka za kawaida, sadaka za kuteketezwa za kawaida, sadaka za siku za Sabato, sikukuu za mwandamo wa mwezi, sikukuu nyingine zilizowekwa, vitu vingine vitakatifu, sadaka za kuondoa dhambi, ili kuwafanyia upatanisho watu wa Israeli na kazi nyingine zozote za nyumba ya Mungu wetu.

34. Sisi sote, watu wote, makuhani na Walawi tutapiga kura kila mwaka ili kuchagua ukoo utakaoleta kuni za kuteketeza tambiko madhabahuni pa Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kama sheria ilivyo.

35. Tunaahidi kuleta kila mwaka malimbuko yetu ya mazao na ya matunda ya kila mti kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu.

Kusoma sura kamili Nehemia 10