Agano la Kale

Agano Jipya

Nahumu 1:7-12 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Mwenyezi-Mungu ni mwema,yeye ni ngome ya usalama wakati wa taabu.Yeye huwalinda wote wanaokimbilia usalama kwake.

8. Adui wakiivamia nchi kama mafuriko, yeye huwaangamiza;huwafuatia na kuwafukuza mpaka gizani.

9. Mbona mnafanya mipango dhidi ya Mwenyezi-Mungu?Yeye atawakomesha na kuwaangamiza,wala mpinzani wake hataweza kuinuka tena.

10. Watateketezwa kama kichaka cha miiba,kama vile nyasi zilizokauka.

11. Kwako kumetoka aliyepanga maovu dhidi ya Mwenyezi-Mungualiyefanya njama za ulaghai.

12. Mwenyezi-Mungu awaambia hivi watu wake:“Ingawa Waashuru ni wengi na wenye nguvu,wao wataangushwa na kuangamizwa.Ingawa nimewatesa nyinyi watu wangu,sitawateseni tena zaidi.

Kusoma sura kamili Nahumu 1