Agano la Kale

Agano Jipya

Nahumu 1:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kauli ya Mungu juu ya Ninewi. Kitabu cha maono ya Nahumu wa Elkoshi.

2. Mwenyezi-Mungu ni Mungu mwenye wivu, mlipiza kisasi;Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi na ni mwenye ghadhabu;Mwenyezi-Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake,huwaka ghadhabu juu ya adui zake.

3. Mwenyezi-Mungu hakasiriki upesi, lakini amejaa nguvu,Mwenyezi-Mungu kamwe hatawaachilia wenye hatia.Apitapo Mwenyezi-Mungu, huzuka kimbunga na dhoruba;mawingu ni vumbi litimuliwalo na nyayo zake.

4. Huikaripia bahari na kuikausha,yeye huikausha mito yote.Mbuga za Bashani na mlima Karmeli hunyauka,maua ya Lebanoni hudhoofika.

5. Milima hutetemeka mbele yake,navyo vilima huyeyuka;dunia hutetemeka mbele yake,ulimwengu na vyote vilivyomo.

6. Nani awezaye kuikabili ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu?Nani awezaye kustahimili ukali wa hasira yake?Yeye huimwaga hasira yake iwakayo kama moto,hata miamba huipasua vipandevipande.

Kusoma sura kamili Nahumu 1