Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 9:9-20 Biblia Habari Njema (BHN)

9. “Ninaweka agano langu nanyi na wazawa wenu

10. na viumbe vyote hai: Ndege, wanyama wa kufugwa na wanyama wa porini, wote waliotoka katika safina pamoja nanyi.

11. Nathibitisha agano langu nanyi, kwamba, kamwe viumbe vyote hai havitaangamizwa kwa gharika, wala haitatokea tena gharika kuiharibu nchi.”

12. Tena Mungu akasema, “Hii ndiyo alama ya agano ninalofanya kati yangu nanyi na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi kwa vizazi vyote vijavyo.

13. Naweka upinde wangu mawinguni, nao utakuwa ishara ya agano kati yangu na dunia.

14. Kila nitakapoifunika dunia kwa mawingu, na huo upinde wa mvua utakapoonekana katika mawingu,

15. nitalikumbuka agano langu nanyi na viumbe vyote hai. Kamwe maji hayatageuka kuwa gharika ya kuviangamiza viumbe vyote hai.

16. Huo upinde utakapotokea mawinguni, nitauona na kulikumbuka agano hilo la milele kati yangu na viumbe vyote hai duniani.”

17. Mungu akamwambia Noa, “Hii ndiyo ishara ya agano ambalo nimefanya na viumbe vyote hai duniani.”

18. Watoto wa Noa waliotoka katika safina walikuwa Shemu, Hamu na Yafethi. Hamu alikuwa baba yake Kanaani.

19. Hao ndio watoto watatu wa Noa, na kutokana nao watu walienea duniani kote.

20. Noa alikuwa mkulima wa kwanza. Alilima shamba la mizabibu,

Kusoma sura kamili Mwanzo 9