Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 9:19-29 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Hao ndio watoto watatu wa Noa, na kutokana nao watu walienea duniani kote.

20. Noa alikuwa mkulima wa kwanza. Alilima shamba la mizabibu,

21. akanywa divai, akalewa, kisha akalala uchi hemani mwake.

22. Hamu, baba yake Kanaani, aliuona uchi wa baba yake, akatoka nje na kuwaambia ndugu zake wawili.

23. Lakini Shemu na Yafethi wakatwaa nguo, wakaitanda mabegani mwao, wakaenda kinyumenyume na kuufunika uchi wa baba yao. Waliangalia pembeni, wala hawakuuona uchi wa baba yao.

24. Noa alipolevuka na kujua alivyotendewa na mwanawe mdogo,

25. akasema,“Kanaani na alaaniwe!Atakuwa mtumwa wa watumwa kwa ndugu zake.”

26. Tena akasema,“Shemu na abarikiwe na Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu!Kanaani na awe mtumwa wake.

27. Mungu na amkuze Yafethi,aishi katika hema za Shemu;Kanaani na awe mtumwa wake.”

28. Baada ya gharika, Noa aliishi miaka 350,

29. kisha akafariki akiwa na umri wa miaka 950.

Kusoma sura kamili Mwanzo 9