Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 8:7-17 Biblia Habari Njema (BHN)

7. akamtoa kunguru nje, naye hakurudi bali aliruka huko na huko mpaka maji yalipokauka nchini.

8. Kisha Noa akamtoa njiwa apate kuona kama maji yalikuwa yamepungua juu ya nchi.

9. Lakini, kwa vile maji yalikuwa bado yameifunika nchi yote, huyo njiwa hakupata mahali pa kutua, akamrudia Noa katika safina. Noa akanyosha mkono, akamtwaa na kumrudisha ndani ya safina.

10. Noa akangoja siku nyingine saba, kisha akamtoa tena huyo njiwa.

11. Njiwa huyo akamrudia Noa saa za jioni akiwa na tawi bichi la mzeituni mdomoni mwake. Kwa hiyo Noa akajua kwamba maji yalikuwa yamepungua katika nchi.

12. Kisha akangoja siku nyingine saba, akamtoa tena yule njiwa; safari hii njiwa hakurudi kabisa.

13. Noa alipokuwa na umri wa miaka 601, siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Noa akafunua kifuniko cha safina na alipotazama, akaona kwamba nchi ilikuwa imekauka.

14. Siku ya 27 ya mwezi wa pili, nchi ilikuwa imekauka kabisa.

15. Hapo, Mungu akamwambia Noa,

16. “Toka katika safina, wewe pamoja na mkeo, wanao na wake zao.

17. Toa pia viumbe wote hai wa kila aina waliokuwa pamoja nawe, ndege na wanyama na kila kiumbe kitambaacho, wapate kuzaa kwa wingi duniani, waongezeke na kuenea kila mahali duniani.”

Kusoma sura kamili Mwanzo 8