Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 7:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Noa akafanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru.

6. Noa alikuwa na umri wa miaka 600 wakati gharika ilipotokea nchini.

7. Noa, mkewe, wanawe na wake zao wakaingia ndani ya safina ili kuiepa gharika.

8. Wanyama walio safi, wanyama walio najisi, ndege na viumbe vyote vitambaavyo,

9. wawiliwawili, dume na jike, wakaingia ndani ya safina pamoja na Noa kama Mungu alivyomwamuru.

10. Baada ya siku saba, maji ya gharika yakaanza kuifunika nchi.

11. Noa alipokuwa na umri wa miaka 600, mnamo siku ya kumi na saba ya mwezi wa pili, siku hiyo chemchemi zote za vilindi vya nchi zikabubujika maji, na madirisha ya mbinguni yakafunguka.

12. Mvua ikanyesha nchini siku arubaini mchana na usiku.

Kusoma sura kamili Mwanzo 7