22. naam, kila kiumbe hai katika nchi kavu kilikufa.
23. Mungu akaangamiza kila kiumbe kilichokuwa hai duniani: Binadamu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Vyote viliangamizwa duniani. Noa tu ndiye aliyesalimika na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.
24. Maji hayo yalidumu katika nchi siku 150.