Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 7:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu akamwambia Noa, “Ingia ndani ya safina wewe pamoja na jamaa yako yote, kwa maana, kati ya watu wote wanaoishi nyakati hizi zako, nimekuona wewe peke yako kuwa mwadilifu mbele yangu.

2. Chukua pamoja nawe wanyama wote walio safi, dume na jike, saba saba; lakini wanyama walio najisi, chukua dume na jike, wawiliwawili.

3. Vilevile chukua ndege wa angani dume na jike, saba saba, ili kuzihifadhi hai aina zao duniani.

4. Baada ya siku saba, nitanyesha mvua nchini siku arubaini mchana na usiku, na kila kiumbe hai nilichokiumba duniani nitakiangamiza.”

5. Noa akafanya yote kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru.

6. Noa alikuwa na umri wa miaka 600 wakati gharika ilipotokea nchini.

7. Noa, mkewe, wanawe na wake zao wakaingia ndani ya safina ili kuiepa gharika.

Kusoma sura kamili Mwanzo 7