Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 6:11-15 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Mungu aliiona dunia kuwa imeharibika na kujaa ukatili.

12. Naam, Mungu aliiangalia dunia, akaona kuwa imeharibika kabisa, kwa maana kila mtu alifuata njia yake mbovu.

13. Mungu akamwambia Noa, “Nimeamua kuwaangamiza binadamu wote kwa sababu wameijaza dunia ukatili. Naam, nitawaangamiza kabisa pamoja na dunia!

14. Kwa hiyo, jitengenezee safina kwa mbao za mpingo. Gawa vyumba ndani yake na ipake lami ndani na nje.

15. Utaitengeneza hivi: Urefu wake mita 139, upana wake mita 25 na kimo chake mita 15.

Kusoma sura kamili Mwanzo 6