Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 5:24-32 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Alikuwa mcha Mungu, akatoweka, kwa maana Mungu alimchukua.

25. Wakati Methusela alipokuwa na umri wa miaka 187, alimzaa Lameki.

26. Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

27. Methusela alifariki akiwa na umri wa miaka 969.

28. Wakati Lameki alipokuwa na umri wa miaka 182, alimzaa mtoto wa kiume.

29. Alimwita mtoto huyo Noa, akisema, “Mtoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika ardhi aliyoilaani Mwenyezi-Mungu.”

30. Baada ya kumzaa Noa, Lameki aliishi miaka 595 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

31. Lameki alifariki akiwa na umri wa miaka 777.

32. Noa alipokuwa na umri wa miaka 500, alimzaa Shemu na Hamu na Yafethi.

Kusoma sura kamili Mwanzo 5