Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 5:22-28 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Henoki alikuwa mcha Mungu. Baada ya kumzaa Methusela, Henoki aliishi miaka 300 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

23. Henoki aliishi miaka 365.

24. Alikuwa mcha Mungu, akatoweka, kwa maana Mungu alimchukua.

25. Wakati Methusela alipokuwa na umri wa miaka 187, alimzaa Lameki.

26. Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

27. Methusela alifariki akiwa na umri wa miaka 969.

28. Wakati Lameki alipokuwa na umri wa miaka 182, alimzaa mtoto wa kiume.

Kusoma sura kamili Mwanzo 5