Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 5:10-29 Biblia Habari Njema (BHN)

10. Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

11. Enoshi alifariki akiwa na umri wa miaka 905.

12. Kenani alipokuwa na umri wa miaka 70, alimzaa Mahalaleli.

13. Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

14. Kenani alifariki akiwa na umri wa miaka 910.

15. Mahalaleli alipokuwa na umri wa miaka 65, alimzaa Yaredi.

16. Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

17. Mahalaleli alifariki akiwa na umri wa miaka 895.

18. Yaredi alipokuwa na umri wa miaka 162, alimzaa Henoki.

19. Baada ya kumzaa Henoki, Yaredi aliishi miaka 800 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

20. Yaredi alifariki akiwa na umri wa miaka 962.

21. Henoki alipokuwa na umri wa miaka 65, alimzaa Methusela.

22. Henoki alikuwa mcha Mungu. Baada ya kumzaa Methusela, Henoki aliishi miaka 300 na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

23. Henoki aliishi miaka 365.

24. Alikuwa mcha Mungu, akatoweka, kwa maana Mungu alimchukua.

25. Wakati Methusela alipokuwa na umri wa miaka 187, alimzaa Lameki.

26. Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, na kupata watoto wengine wa kiume na wa kike.

27. Methusela alifariki akiwa na umri wa miaka 969.

28. Wakati Lameki alipokuwa na umri wa miaka 182, alimzaa mtoto wa kiume.

29. Alimwita mtoto huyo Noa, akisema, “Mtoto huyu ndiye atakayetufariji kutokana na kazi yetu ngumu tunayofanya kwa mikono yetu katika ardhi aliyoilaani Mwenyezi-Mungu.”

Kusoma sura kamili Mwanzo 5