Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 49:7-17 Biblia Habari Njema (BHN)

7. “Nalaani hasira yao maana ni kali mno,na ghadhabu yao isiyo na huruma.Nitawatawanya katika nchi ya Yakobo,nitawasambaza katika nchi ya Israeli.

8. “Wewe Yuda, ndugu zako watakusifu.Adui zako utawakaba shingo;na ndugu zako watainama mbele yako.

9. “Wewe Yuda, mwanangu, ni kama mwanasimbaambaye amepata mawindo yake akapanda juu.Kama simba hujinyosha na kulala chini;simba mwenye nguvu, nani athubutuye kumwamsha?

10. “Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda,wala bakora ya utawala miguuni pake,mpaka atakapofika yule ambaye ni yake;ambaye mataifa yatamtii.

11. “Atafunga punda wake katika mzabibuna mwanapunda wake kwenye mzabibu bora.Hufua nguo zake katika divai,na mavazi yake katika divai nyekundu.

12. “Macho yake ni mekundu kwa divai,meno yake ni meupe kwa maziwa.

13. “Zebuluni ataishi sehemu za pwani,pwani yake itakuwa mahali pa kuegesha meli.Nchi yake itapakana na Sidoni.

14. “Isakari ni kama punda mwenye nguvu,ajilazaye kati ya mizigo yake.

15. “Aliona kuwa mahali pa kupumzikia ni pema,na kwamba nchi ni ya kupendeza,akauinamisha mgongo wake kubeba mzigo,akawa mtumwa kufanya kazi za shuruti.

16. “Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake,kama mojawapo ya makabila ya Israeli.

17. “Atakuwa kama nyoka njiani,nyoka mwenye sumu kando ya njia,aumaye visigino vya farasi,naye mpandafarasi huanguka chali.

Kusoma sura kamili Mwanzo 49