Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 49:23-27 Biblia Habari Njema (BHN)

23. “Wapiga mishale walimshambulia vikali,wakamtupia mishale na kumsumbua sana.

24. “Lakini upinde wake bado imara,na mikono yake imepewa nguvu,kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli;

25. “kwa Mungu wa baba yako atakayekusaidia,kwa Mungu mwenye nguvu atakayekubariki;upate baraka za mvua toka juu mbinguni,baraka za maji ya vilindi vilivyo chini,baraka za uzazi wa akina mama na mifugo.

26. Baraka za baba yako zishinde baraka za milima ya milele,ziwe bora kuliko vilima vya kale.Baraka hizo na ziwe juu ya kichwa cha Yosefu,juu ya paji lake yeye aliyekuwa ametengwa na ndugu zake.

27. “Benyamini ni mbwamwitu mkali;asubuhi hula mawindo yake,na jioni hugawa nyara.”

Kusoma sura kamili Mwanzo 49