Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 49:15-24 Biblia Habari Njema (BHN)

15. “Aliona kuwa mahali pa kupumzikia ni pema,na kwamba nchi ni ya kupendeza,akauinamisha mgongo wake kubeba mzigo,akawa mtumwa kufanya kazi za shuruti.

16. “Dani atakuwa mwamuzi wa watu wake,kama mojawapo ya makabila ya Israeli.

17. “Atakuwa kama nyoka njiani,nyoka mwenye sumu kando ya njia,aumaye visigino vya farasi,naye mpandafarasi huanguka chali.

18. “Ee Mwenyezi-Mungu, nangojea uniokoe!

19. “Gadi atashambuliwa na wanyanganyi,lakini yeye atawafuata nyuma na kuwashambulia.

20. “Ardhi ya Asheri itatoa mavuno kwa wingi,naye atatoa chakula kimfaacho mfalme.

21. “Naftali ni kama paa aliye huru,azaaye watoto walio wazuri.

22. “Yosefu ni kama mti uzaao,mti uzaao kando ya chemchemi,matawi yake hutanda ukutani.

23. “Wapiga mishale walimshambulia vikali,wakamtupia mishale na kumsumbua sana.

24. “Lakini upinde wake bado imara,na mikono yake imepewa nguvu,kwa uwezo wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,kwa jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli;

Kusoma sura kamili Mwanzo 49