Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 46:4-17 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Mimi mwenyewe nitakwenda pamoja nawe huko Misri na kukurudisha huku. Utakapofariki, mkono wa Yosefu ndio utakaoyafumba macho yako.”

5. Basi, Yakobo akaondoka Beer-sheba. Wanawe wakamchukua yeye, watoto wao wachanga pamoja na wake zao katika magari ambayo Farao alipeleka kumchukua.

6. Walichukua pia mifugo na mali yao yote waliyokuwa wamechuma katika nchi ya Kanaani, wakaenda Misri. Yakobo aliwachukua wazawa wake wote:

7. Wanawe, wajukuu wake wa kiume na wa kike, wote akawaleta Misri.

8. Wazawa wa Israeli ambao walikwenda Misri pamoja naye walikuwa Reubeni, mzaliwa wake wa kwanza,

9. pamoja na wana wa Reubeni: Henoki, Palu, Hesroni na Karmi.

10. Simeoni na wanawe: Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli, aliyezaliwa na mwanamke Mkanaani.

11. Lawi na wanawe: Gershoni, Kohathi na Merari.

12. Yuda na wanawe: Eri, Onani, Shela, Peresi na Zera. (Lakini Eri na Onani walifariki katika nchi ya Kanaani). Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli.

13. Isakari na wanawe: Tola, Puva, Yashubu na Shimroni.

14. Zebuluni na wanawe: Seredi, Eloni na Yaleeli.

15. Hao ndio wana ambao Lea alimzalia Yakobo kule Padan-aramu, pamoja na Dina binti yake. Jumla ya wanawe, binti zake na wajukuu wake walikuwa watu thelathini na watatu.

16. Gadi na wanawe: Sifioni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi na Areli.

17. Asheri na wanawe: Imna, Ishva, Ishvi, Beria na Sera, dada yao. Beria na wanawe: Heberi na Malkieli.

Kusoma sura kamili Mwanzo 46