Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 41:17-26 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Hapo Farao akamwambia Yosefu, “Niliota kwamba nimesimama kando ya mto Nili,

18. nikaona ng'ombe saba wazuri na wanono wakitoka mtoni na kula nyasi.

19. Hao wakafuatwa na ng'ombe wengine saba dhaifu, wembamba na wamekonda sana. Mimi sijapata kamwe kuona ng'ombe wa hali hiyo katika nchi ya Misri.

20. Basi, wale ng'ombe waliokonda sana wakawala wale ng'ombe saba wanono.

21. Lakini hata baada ya kuwala wale wanono, mtu yeyote asingeweza kutambua kwamba wamewala wenzao, kwani bado walikuwa wamekondeana kama mwanzo. Hapo nikaamka usingizini.

22. Kisha nikaota ndoto nyingine: Niliona masuke saba mazuri yaliyojaa nafaka yakichipua katika bua moja.

23. Halafu yakafuatwa na masuke mengine saba matupu, membamba na yaliyokaushwa na upepo mkavu wa jangwani.

24. Yale masuke saba membamba yakayameza yale masuke saba mazuri. Basi, mimi niliwaambia wachawi ndoto hizo lakini hakuna mtu aliyeweza kunifafanulia.”

25. Ndipo Yosefu akamwambia Farao, “Ndoto zako zote mbili tafsiri yake ni moja. Mungu amekufunulia mambo atakayofanya hivi karibuni.

26. Ngombe wale saba wazuri ni miaka saba, na yale masuke saba mazuri pia ni miaka saba; ndoto hiyo tafsiri yake ni moja.

Kusoma sura kamili Mwanzo 41