Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 4:22-26 Biblia Habari Njema (BHN)

22. Sila naye alimzaa Tubal-kaini, ambaye alikuwa mhunzi wa vyombo vyote vya shaba na chuma. Dada yake Tubal-kaini alikuwa Naama.

23. Lameki akawaambia wake zake,“Ada na Sila sikieni sauti yangu!Sikilizeni nisemayo enyi wake za Lameki.Mimi niliua mtu kwa kunijeruhi,naam, nilimuua kijana kwa kuniumiza.

24. Ikiwa Kaini atalipizwa mara saba,kweli Lameki atalipizwa mara sabini na saba.”

25. Adamu akalala tena na Hawa mkewe, naye akazaa mtoto wa kiume, akamwita Sethi akisema, “Mungu amenijalia mtoto mahali pa Abeli aliyeuawa na Kaini.”

26. Sethi naye alipata mtoto wa kiume, akamwita Enoshi. Hapo ndipo watu walipoanza kumwomba Mwenyezi-Mungu kwa jina lake.

Kusoma sura kamili Mwanzo 4