Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 36:7-21 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Alifanya hivyo kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi hata wasiweze kuishi pamoja. Nchi waliyokaa kama wageni haikuweza kuwatosha kwa sababu ya wingi wa mifugo yao.

8. Kwa hiyo, Esau akaenda kukaa katika nchi ya milima ya Seiri. Jina lingine la Esau ni Edomu.

9. Wafuatao ni wazawa wa Esau, baba ya Waedomu katika nchi ya milima ya Seiri.

10. Watoto wa kiume wa Esau walikuwa Elifazi aliyezaliwa na Ada mkewe, na Reueli aliyezaliwa na Basemathi mke wake mwingine.

11. Watoto wa kiume wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi.

12. Elifazi alikuwa na suria jina lake Timna. Huyu alimzalia mwana, jina lake Amaleki.

13. Basemathi, mkewe Esau, alimzaa Reueli. Watoto wa kiume wa Reueli walikuwa Nahathi, Zera, Shama na Miza.

14. Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, alimzalia Esau mumewe watoto wa kiume watatu: Yeushi, Yalamu na Kora.

15. Wafuatao ni wakuu wa makabila yaliyotokana na Esau. Elifazi, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Esau aliwazaa Temani, Omari, Sefo, Kenazi,

16. Kora, Gatamu na Amaleki, kila mmoja wao akiwa mkuu wa kabila lake. Hao wote ni watoto wa kiume wa Elifazi katika nchi ya Edomu, waliotokana na Ada, mkewe Esau.

17. Reueli, mwanawe Esau, aliwazaa Nahathi, Zera, Shama na Miza, kila mmoja wao akawa mkuu wa kabila lake. Hao wote ni watoto wa kiume wa Reueli katika nchi ya Edomu, waliotokana na Basemathi, mkewe Esau.

18. Watoto wa kiume wa Oholibama, mkewe Esau, walikuwa Yeushi, Yalamu na Kora, kila mmoja wao akiwa mkuu wa kabila lake. Hao wote ni watoto wa kiume wa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau.

19. Basi, hao ndio wazawa wa Esau yaani Edomu, kila mmoja wao akiwa mkuu wa kabila lake.

20. Wafuatao ni wazawa wa Seiri, Mhori, na ndio wenyeji wa nchi hiyo: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,

21. Dishoni, Eseri na Dishani; kila mmoja wao akiwa mkuu wa kabila lake miongoni mwa Wahori wa uzawa wa Seiri, katika nchi ya Edomu.

Kusoma sura kamili Mwanzo 36