Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 36:32-43 Biblia Habari Njema (BHN)

32. Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba.

33. Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra alitawala badala yake.

34. Yobabu alipofariki, Hushamu wa nchi ya Watemani, alitawala badala yake.

35. Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi alitawala badala yake, makao yake makuu yakiwa katika mji wa Avithi. Huyu ndiye aliyewapiga na kuwashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu.

36. Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka, alitawala badala yake.

37. Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi, ulio karibu na mto Eufrate, alitawala badala yake.

38. Shauli alipofariki, Baal-hanani, mwana wa Akbori, alitawala badala yake.

39. Baal-hanani, mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi alitawala badala yake, na jina la mji wake likiwa Pau. Mkewe Akbori alikuwa Mehetabeli, binti Matredi na mjukuu wa Mezahabu.

40. Wakuu wa makabila yaliyotokana na Esau, kadiri ya makabila yao na makazi yao walikuwa: Timna, Alva, Yethethi,

41. Oholibama, Ela, Pinoni,

42. Kenazi, Temani, Mibsari,

43. Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila yaliyotokana na Edomu, yaani Esau, baba yake Edomu; wametajwa kulingana na makazi yao katika sehemu za nchi walizomiliki.

Kusoma sura kamili Mwanzo 36