Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 36:25-37 Biblia Habari Njema (BHN)

25. Watoto wa Ana walikuwa Dishoni na dada yake mmoja aitwaye Oholibama.

26. Watoto wa kiume wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

27. Watoto wa kiume wa Eseri walikuwa Bilhani Zaawani na Akani.

28. Watoto wa kiume wa Dishani walikuwa Usi na Arani.

29. Basi, hao ndio wakuu wa Wahori: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,

30. Dishoni, Eseri na Dishani; kila mmoja wao akiwa mkuu wa kabila lake katika nchi ya Seiri.

31. Wafuatao ni wafalme waliotawala nchi ya Edomu, kabla mfalme yeyote hajawatawala Waisraeli:

32. Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba.

33. Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra alitawala badala yake.

34. Yobabu alipofariki, Hushamu wa nchi ya Watemani, alitawala badala yake.

35. Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi alitawala badala yake, makao yake makuu yakiwa katika mji wa Avithi. Huyu ndiye aliyewapiga na kuwashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu.

36. Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka, alitawala badala yake.

37. Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi, ulio karibu na mto Eufrate, alitawala badala yake.

Kusoma sura kamili Mwanzo 36