Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 36:24-31 Biblia Habari Njema (BHN)

24. Watoto wa kiume wa Sibeoni walikuwa Aya na Ana. Ana ndiye aliyeziona chemchemi za maji ya moto jangwani, alipokuwa anawachunga punda wa baba yake Sibeoni.

25. Watoto wa Ana walikuwa Dishoni na dada yake mmoja aitwaye Oholibama.

26. Watoto wa kiume wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.

27. Watoto wa kiume wa Eseri walikuwa Bilhani Zaawani na Akani.

28. Watoto wa kiume wa Dishani walikuwa Usi na Arani.

29. Basi, hao ndio wakuu wa Wahori: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,

30. Dishoni, Eseri na Dishani; kila mmoja wao akiwa mkuu wa kabila lake katika nchi ya Seiri.

31. Wafuatao ni wafalme waliotawala nchi ya Edomu, kabla mfalme yeyote hajawatawala Waisraeli:

Kusoma sura kamili Mwanzo 36