Agano la Kale

Agano Jipya

Mwanzo 35:17-23 Biblia Habari Njema (BHN)

17. Naye alipokuwa katika uchungu huo, mkunga akamwambia, “Usiogope, umepata mtoto mwingine wa kiume.”

18. Raheli huku akikata roho, akampa huyo mtoto jina Ben-oni. Lakini baba yake akamwita mtoto huyo Benyamini.

19. Basi, Raheli akafariki na kuzikwa kando ya njia iendayo Efratha (yaani Bethlehemu).

20. Yakobo akasimika nguzo ya kumbukumbu juu ya kaburi la Raheli ambayo ipo mpaka leo.

21. Israeli akaendelea na safari yake na kupiga kambi yake baada ya kuupita mnara wa Ederi.

22. Wakati Israeli alipokuwa anakaa nchini humo, mwanawe Reubeni, alilala na Bilha, suria wa baba yake; naye Israeli akasikia habari hizo.Yakobo alikuwa na watoto wa kiume kumi na wawili.

23. Wana wa Lea walikuwa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari na Zebuluni.

Kusoma sura kamili Mwanzo 35